Wiki iliyopita, Mbunge wa chama cha Republican na mpambe wa rais Trump Cory Mills alikutana na kufanya mazungumzo na al-Jolani mjini Damascus kwa muda wa dakika 90 katika safari ya kutafuta ukweli iliyofadhiliwa na Wamarekani wenye asili ya Syria.
Kwa mujibu wa Mills, Syria iko tayari kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Israel na kujiunga na Mkataba wa Abraham, lakini "kwa masharti sahihi".
Mills amesema, msimamo huo umeelezwa na al-Jolani katika mazungumzo hayo wakati alipoomba kupatiwa msamaha wa vikwazo ilivyowekewa Syria na madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani na kuzungumzia pia uvamizi wa kijeshi na ukaliaji ardhi kwa mabavu uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kusini magharibi mwa Syria.
Mbunge huyo wa Marekani ameiambia Bloomberg kwamba alijadiliana na al-Jolani kuhusu hatua anazohitajiwa kuzichukua yeye al-Jolani ili kupata msamaha wa vikwazo.
Amesema alimueleza al-Jolani kuwa Syria lazima iteketeze silaha za kemikali zilizoachwa na serikali ya Bashar al-Assad, ishirikiane na nchi jirani katika kukabiliana na ugaidi na kupambana pia na wapiganaji wa kigeni waliojaa kwenye safu za kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS).
Aidha, Mills alimtaka kiongozi huyo wa kundi la HTS atoe hakikisho la usalama kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.../
342/
Your Comment